Kocha wa timu ya taifa ya Hispania ametangaza kikosi kitakachotumika katika michezo ijayo ya UEFA Nations League, kikiwa na nyota mbalimbali wanaocheza katika klabu kubwa barani Ulaya.
Katika nafasi ya makipa, walioitwa ni Unai Simón, David Raya, Joan García na Álvaro Valles. Safu ya ulinzi inaundwa na Laporte, Cubarsí, Marc Pubill, Huijsen, Pedro Porro, Jacobo Ramón, Cucurella na Grimaldo.
Kwa upande wa kiungo, Hispania imewaita Fabián Ruiz, Pedri, Merino, Zubimendi, Álex Baena, Fermín López, Pablo Barrios na Marc Roca.
Katika safu ya ushambuliaji wamo Oyarzabal, Ferran Torres, Roberto Fernández, Lamine Yamal, Nico Williams, Yeremy Pino na Ander Barrenetxea.
Hispania sasa inaelekeza nguvu zake katika maandalizi ya michezo hiyo ya Nations League, huku ikitarajia kutumia ubora wa kikosi hicho kuendelea kufanya vizuri katika mashindano hayo.