Pochettino kuanza rasmi kazi Manchester United Novemba 18, akijiandaa na mtihani wa Liverpool

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
3d ago
Pochettino kuanza rasmi kazi Manchester United Novemba 18, akijiandaa na mtihani wa Liverpool

Kocha Mauricio Pochettino anatarajiwa kuanza rasmi majukumu yake kama kocha mkuu wa Manchester United kesho, Novemba 18, baada ya kukamilisha majukumu yake ya mwisho akiwa na timu ya taifa ya Marekani.

Pochettino amechaguliwa kuiongoza United akichukua nafasi ya Michael Carrick, ambaye alifutwa kazi wiki iliyopita kufuatia mwenendo usioridhisha wa timu hiyo katika Ligi Kuu England.

Kocha huyo raia wa Argentina anakabiliwa na kazi kubwa ya kuirejesha United kwenye ushindani baada ya timu hiyo kushinda mchezo mmoja pekee kati ya michezo 10 ya mwanzo ya ligi na kujikuta katika nafasi ya 18 kwenye msimamo.

Kabla ya kuanza kazi Old Trafford, Pochettino anapaswa kumaliza majukumu yake na Marekani katika michezo miwili dhidi ya Haiti ya Concacaf Nations League. Baada ya mchezo wa mwisho, anatarajiwa kusafiri kwa ndege binafsi kwenda Manchester na kuwasili Jumatano asubuhi.

Anatarajiwa kuelekea moja kwa moja katika kituo cha mazoezi cha Carrington kuanza maandalizi ya mchezo wake wa kwanza dhidi ya Liverpool utakaopigwa Jumapili katika dimba la Anfield.

Baada ya Liverpool, Pochettino pia atakabiliwa na michezo dhidi ya Sporting CP na Brentford, ikiwa ni mwanzo wa safari yake ya kujaribu kuibadilisha Manchester United ambayo imekuwa na mwanzo mgumu wa msimu.

More Stories

Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
6h ago
READ MORE β†’
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
11h ago
READ MORE β†’
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
12h ago
READ MORE β†’
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
14h ago
READ MORE β†’
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
14h ago
READ MORE β†’
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
15h ago
READ MORE β†’
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
16h ago
READ MORE β†’
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
17h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
20h ago
READ MORE β†’