Hardrock FC imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Zimbabwe ya Castle Lager msimu wa 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya FC Platinum katika mchezo wa mwisho wa ligi.
Shujaa wa Hardrock FC alikuwa mshambuliaji Prince Dube, aliyefunga bao pekee la mchezo dakika ya kwanza tu na kuhakikisha timu yake inapata pointi tatu muhimu za kutwaa ubingwa.
Katika mchezo mwingine uliokuwa ukiamua hatma ya ubingwa, Scottland iliichapa Triangle United mabao 2-1, lakini matokeo hayo hayakutosha kuinyima Hardrock FC taji hilo.
Ikumbukwe kuwa Prince Dube alijiunga na Hardrock FC katika dirisha lililopita la usajili akitokea Young Africans SC ya Tanzania, na sasa ameisaidia timu yake mpya kutwaa ubingwa wa Zimbabwe.
Hongera Hardrock FC kwa kutwaa taji la msimu wa 2026.