Klabu ya Al Ahly ya Misri imemfuta kazi kocha wake mkuu, Hussein Ammouta, pamoja na wasaidizi wake, ikiwa ni muda mfupi baada ya timu hiyo kupoteza mchezo dhidi ya Pyramids FC.
Ammouta, ambaye ni raia wa Morocco, alijiunga na mabingwa hao wa Afrika Juni 8, 2026, kwa mkataba wa miaka miwili, akichukua nafasi ya kocha Mdenmark Jess Thorup.
Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa rasmi wa klabu hiyo, Al Ahly imetoa shukrani kwa Ammouta na benchi lake la ufundi kwa mchango wao katika kipindi chote walichokuwa wakihudumu, huku ikieleza kuwa hatua hiyo imefuatia maamuzi ya viongozi wanaosimamia idara ya soka.
Aidha, Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Yassin Mansour, pamoja na mjumbe wa bodi, Sayed Abdel Hafeez, wamepewa jukumu la kuandaa orodha ya makocha wanaoweza kuchukua nafasi hiyo na kuiwasilisha ndani ya saa chache zijazo.