Ajib kutua Yanga ni habari nyingine mbaya kwa wale wa upande uleee

Admin By Admin
β€’
5 Jul 2017
Ajib kutua Yanga ni habari nyingine mbaya kwa wale wa upande uleee
Baada ya kuvumishwa sana kuwa Yanga 'salio limekata' sasa ni dhahiri wale wote waliokuwa wakiropoka maneno hayo wanatafuta pa kujificha.

Najua kuna baadhi ya magazeti na vyombo vya habari vilikuwa vimepewa 'kazi maalum' ya kuchafua hali ya hewa Jangwani ili wachezaji tuliokuwa tunawawania waingie mitini kuhofia njaa.

Walifanikiwa kwa baadhi ya wachezaji tuliowataka mwanzoni, lakini nina uhakika wale wachezaji waliotutosa siku za mwanzo za usajili wanajilaumu sasa hivi. Walipiga teke bahati!

Leo tumemshuhudia Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwassa 'Master' akitutambulishia jembe la uhakika, Ibrahim Ajib.



Nawaambieni wana Jangwani, miguu ya huyu jamaa ina mabao mengi sana. Wakati yuko Simba hakupata fursa ya kuonyesha kipaji chake ipasavyo kutokana na aina ya wachezaji walioko pale.

Huku kwetu tuna mafundi wa kupika mabao, tunae Thabani Kamusoko hata kama Niyonzima asipokuwepo, atakuwepo Raphael Daudi.

Pia Obrey Chirwa licha ya kuwa miongoni mwa wafungaji hodari, nae ni mtengenezaji mzuri sana wa mabao.

Sipachi picha itakuwaje pale Donald Ngoma, Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa wakiongoza mashambulizi pale mbele! Hapo hatujamuweka Amissi Tambwe 'mabao'.

Msuva tunaweza tusiwe nae, kama amepata timu nje aende ni vizuri hatuna sababu ya kumuharibia 'future' yake kwani mpira ndio kazi yake.

Lakini najua uongozi wa Yanga utaleta majembe imara yatakayofanya kazi zaidi ya aliyokuwa anafanya Msuva.

Habari ziwafikie huko waliko, Agosti 19 sio mbali, itatafahamika tu mapemaaaa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’