Mashabiki Yanga hawamwamini Dimpoz, GSM mmesikia?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Mar 2021
Mashabiki Yanga hawamwamini Dimpoz, GSM mmesikia?

Yanga na Simba ni timu zenye upinzani wa asili, hizi timu zina utamaduni wake ambao uko tofauti sana na vilabu vingine vyenye upinzani wa jadi kote duniani

Ni hivi; ukiwa shabiki wa Simba ni haramu kuajiriwa pale Yanga lakini pia ni hivyo hivyo mtu wa Yanga hawezi kufanya kazi Simba

Viongozi wengi wameingia matatani kwa kushukiwa tu ni shabiki wa timu ya upande wa pili, hizi timu zinapendwa sana, mashabiki hawako tayari kufanya kazi na yeyote wa upande wa pili kuhofia hujuma

Mitandaoni, kumekuwa na maoni ya mashabiki wa Yanga ambao hawafurahii kile kinahofanywa na Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Ommy Dimpoz ambaye anafahamika kuwa 'mnazi lialia' wa Simba

Dimpoz ni mwajiriwa wa GSM kama balozi, anafanya shughuli mbalimbali za kutangaza bidhaa za GSM. Huyu ni mwajiriwa wa GSM, sio Yanga

Lakini kwa kutumia kofia yake hiyo, kwa nyakati tofauti Dimpoz amepata nafasi ya kujumuika na viongozi waandamizi na hata wachezaji wa Yanga

GSM wanaidhamini Yanga, wameshiriki kusajili, na wanalipa mishahara ya wachezaji. Zipo nyakati wachezaji wanakutana na waajiriwa wengine wa GSM 'koridoni'

Mashabiki wameonyesha kutofurahishwa na uhuru ambao Dimpoz amepewa kwani mara nyingi ameonekana akiwa na wachezaji wa Yanga

Wananchi bado hawajasahau, kilichotokea kwa Morrison. Yapo maoni ya wengi ambao wanadhani GSM wanakosea sana

Kwa sababu huyu ni mshabiki wa Simba ambaye dakika yoyote anaweza kukutana na akina Mukoko, Kisinda, Fiston na nyota wengine hasa wa kigeni

Jimmy Kindoki ni mhamasishaji na Mwanachama maarufu wa Yanga yeye ameshauri GSM wangempa Dimpoz majukumu mengine ambayo hayatawaweka mashabiki katika shaka

"Mimi nishauri tu Ommy angepewa majukumu mengine kwasababu tayari wanayanga hawana imani nae tena"," aliandika Ommy katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Lakini pia wapo wanaoamini kuwa mchakato wa Mabadiliko ukikamilika haraka, utaondoa hizi changamoto

Kwa sasa GMS ni mhisani tu Yanga, ana biashara zake ambazo ni haki yake kuajiri mtu yeyote

Kama GSM akiwa mwekezaji Yanga, mambo haya hayatakuwepo kwani atafanya kazi sambamba na kampuni itakayoundwa na Wanayanga wenyewe

Wachezaji wote watakuwa chini ya umiliki mmoja na sintofahamu inayoonekana sasa haitakuwepo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’