Mlinda lango wa Yanga Farouk Shikhalo amesema kwa aina ya mazoezi ambayo kocha Juma Mwambusi anawapatia, muda sio mrefu, watarejea katika ubora wao
Tangu kuanza majukumu yake kama Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Mwambusi amewaongezea wachezaji 'dozi' ya mazoezi
Shikhalo amemsifu Mwambusi kuwa anafahamu mahitaji ya Yanga na uzoefu wake ndani ya timu na kwenye ligi ni faida kwake
"Tulikuwa naye kabla, wachezaji takribani wote tunamfahamu na alivyoanza binafsi naona ni kocha mzuri sana, nathubutu kusema ubora wa kikosi utarejea haraka," Shikhalo amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti
"Hii ratiba ya mazoezi ya mara mbili kwa siku anaonyesha ni kocha ambaye sio tu anaijua Yanga ambacho inataka bali kinachohitajika katika ushindani wa timu za ligi"

Mlinda lango huyo wa zamani klabu ya Bandari Fc ya Kenya, amesema Mwambusi ana muda wa kutosha kurejesha ubora wa kikosi chake
"Tuna siku kama 20 hapa kabla ligi haijaendelea, hiki kipindi kinaweza kumsaidia sana kurudisha ubora wa timu kwa kuwa hakuna presha ya kuingia katika mechi za mashindano"
Mchezo wake wa kwanza ni dhidi ya Tanzania Prisons, kombe la FA ambao utapigwa April 04 mkoani Rukwa uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga