Washambuliaji Yanga mtegoni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Mar 2021
Washambuliaji Yanga mtegoni

Safu ya ushambuliaji ya Yanga msimu huu imeshindwa kuwapa furaha mashabiki kutokana na mwenendo mbovu wa kuzifumania nyavu

Mabadiliko ya kumuondoa kocha Cedric Kaze yalikuwa ya pili kufanywa na uongozi wa Yanga yote ikiwa ni jitihada ya kusaka tiba ya changamoto zilizokuwepo

Ubutu wa safu ya ushambuliaji ndio kilio cha mashabiki jambo lililopelekea hata wengine kupoteza imani kwa baadhi ya washambuliaji kuwa hawakustahili kusajiliwa na Yanga

Mghana Michael Sarpong ndiye mhanga mkuu wa ukosoaji kasi yake ya kuzifumania nyavu ikiwa hairidhishi

Wakati Yanga ikinolewa na Zlatko Krmpotic, Sarpong alianza msimu vyema akifunga bao katika mchezo wa kwanza kabisa dhidi ya Tanzania Prisons

Hilo lilikuwa bao pekee alilofunga katika michezo mitano ambayo Krmpotic aliiongoza Yanga

Katika michezo 18 chini ya kocha Cedric Kaze, Sarpong alifunga mabao matatu tu pamoja na kuwa zipo nyakati alikosekana uwanjani kutokana na majeruhi

Washambuliaji wengine, Waziri Junior yeye alifunga bao moja wakati wa Kaze, Yacouba Songne ndiye mshambuliaji aliyeng'ara zaidi wakati wa Kaze, akifunga mabao matatu na kutoa pasi nne za mabao. Alifunga bao moja wakati wa Krmpotic

Fiston Abdulrazak yeye alitua katika usajili wa dirisha dogo na amefanikiwa kufunga bao moja

Katika michezo 11 iliyosalia kwenye ligi na kombe la FA, washambuliaji hawa wanapaswa kudhihirisha ubora wao ili mabosi wa Yanga wapate sababu ya kuendelea nao msimu ujao

Kama hakutakuwa na mabadiliko ni wazi panga kali la mwishoni mwa msimu linaweza kuwapitia

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’