Baada ya kukabidhiwa Kamati ya Mashindano, Nyika aeleza mikakati yake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
18 Dec 2017
Baada ya kukabidhiwa Kamati ya Mashindano, Nyika aeleza mikakati yake
Kamati ya Mashindano ambayo sasa inaongozwa na Hussein Nyika imepewa jukumu jipya la kuhakikisha timu inafanya vema katika kila mechi iwe ya Ligi Kuu Bara, Kombe la FA, Kombe la Mapinduzi ama ile ya Afrika, ambapo mwakani kwa mara nyingine Yanga itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mahojiano yake na gazeti la Mwanaspoti hivi karibuni, Nyika ambaye amepwea jukumu la kuongoza kamati hiyo, mbali na kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, alisema anajua jukumu alilopewa ni zito ila kwa wajumbe alionao haoni sababu ya Yanga kushindwa kutetea taji lao la ubingwa wa Bara msimu huu.

Nyika alisema hata kabla hajapewa jukumu hilo, alikuwa katika kamati hiyo kama mjumbe ambapo suala la kutetea taji lao la ubingwa wa Ligi Kuu Bara ni kitu kisichoepukika na watafanya kweli licha ya Simba kuongoza msimamo kwa sasa.

Alisema, mbali na kupiga hesabu kali za kuona Yanga wanatetea taji lao, lakini pia mikakati yao mingine ni kurejesha taji la FA waliotemeshwa katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Mbao FC na kujipanga kwa mechi ya Ligi ya Mabingwa.

“Kwa namna tulivyojipanga yeyote akija mbele yetu, lazima tumnyooshe kwa sababu tumepania kuwafunga mdomo wote wanaosema vibaya dhidi yetu, iwe ni Simba ama Waarabu tutakaojileta kwenye angaza zetu Afrika,” alisema.



Nyika alisema jambo ambalo wamekubaliana na Kocha Mkuu wa Yanga, Mzambia George Lwandamina ni kuhakikisha katika mechi nne za awali za Ligi ya Mabingwa (yaani za raundi ya awali na kwanza) wanashinda ili watinge hatua ya makundi.

“Ninaposema tunautaka ubingwa kauli hiyo inakwenda na mikakati mizito ambayo kamati tulishaiweka tunajua sasa ndio ligi inaongozwa na Simba, lakini haijaisha kwani, tofauti ya pointi ni mbili. Wanayanga watupe nafasi tufanye kazi.

“Tunajua pia mipango yetu hatuangalii ligi tu tunataka mashindano mengine yote tuwe na ushiriki bora nimeona watu wanatubeza, eti hatutakuwa na jipya katika Ligi ya Mabingwa. Wasubiri waone kwani safari hii tunakuja kivingine.

“Tuna kocha bora na kikosi kizuri chenye muunganiko wa wachezaji wenye uzoefu wa kutosha, endapo Mungu atatusaidia kwa kila mchezaji kuwa na afya bora hakuna timu inayotupa wasiwasi katika ratiba ambayo tumeiona,” alisema Nyika na kuongeza kwa kujiamini;

“Hakuna kinachoshindikana katika kupata ushindi japo tunawaheshimu wapinzani wetu, ila kamati yangu haitaogopa timu yoyote tumeshawafunga Waarabu hivi karibuni tu, hivyo hatuna sababu ya kuhofia kukutana na yeyote Afrika.”

Yanga imepangwa kuanza mechi zake za awali dhidi ya St Louis ya Shelisheli kati ya Februari 9-18 na kama itafuzu katika raundi ya kwanza basi huenda ikakutana ama na El Merreikh ya Sudan au Township Rollers ya Botswana.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →