Kiungo mshambuliaji wa Yanga Saido Ntibazonkiza yuko katka kikosi cha timu ya Taifa ya Burundi kinachojiandaa na mechi za kuwania kufuzu fainali za Afcon 2021 mwishoni mwa mwezi huu
Kwa muda mrefu Ntibazobkiza alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya misuli na nyonga
Ntibazonkiza alianza kusumbuliwa na maumivu hayo baada ya mchezo dhidi ya Ihefu Fc
Alicheza mechi dhidi ya Prisons na fainali ya kombe la Mapinduzi dhidi ya Simba akiwa bado anasumbuliwa na majeraha hayo
Nyota huyo alianza kutibiwa jijini Dar es salaam na akaruhusiwa kurejea kwao Burundi kuendelea na matibabu
Saido sasa yuko fiti kwa asilimia 100 na atajiunga na kikosi cha Yanga baada ya mechi za kuwania kufuzu Afcon kumalizika
ADVERTISE HERE