Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wanawashukuru wadhamini wao wakuu kampuni ya Sportpesa ambao wako mwishoni mwa mkataba wao
Mwezi Juni mwaka huu Mkataba wa Sportpesa na Yanga utafikia mwisho huku kukiwa na nafasi ya pande mbili kusaini mkataba mwingine
Wakati watani zao Simba kupitia Mwekezaji wao Mohammed Dewji akiweka wazi kusudio la kuachana na Sportpesa pale mkataba wao utakapomalizika, Bumbuli amebainisha kuwa wanajivunia udhamini huo huku akimpiga 'dongo' Mo
"Ukiona mtu hawezi kushukuru kwa kidogo, basi hata akipewa kikubwa hawezi Kushukuru. AHSANTE Sana Sportpesa heri KENDA NENDA kuliko 20 naniliu za kusubiri miaka na miaka," aliandika Bumbuli kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Yanga imekuwa ikipokea takribani Tsh Bilioni Moja kila mwaka kutoka kwa SportPesa wakisaini mkataba wa miaka mitano mwishoni mwa msimu wa 2016/17