Muguna ahusishwa na Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Mar 2021
Muguna ahusishwa na Yanga

Mwishoni mwa mwezi May, msimu wa ligi kuu ya Vodacom 2020/21 utafika tamati na kukaribisha msimu mwingine 2021/22

Tayari tetesi za usajili zimeanza kushika kasi timu zikianza kuangalia wachezaji wanaoweza kuwajumuisha kuongeza nguvu katika vikosi vyao kwa ajili ya msimu ujao

Yanga imekuwa na msimu mzuri mpaka sasa licha ya maboresho makubwa yaliyofanyika msimu uliopita

Wananchi waliongeza wachezaji 17 wapya, bado maboresho mengine yatafanyika mwishoni mwa msimu huu

Ndio maana tetesi zimeanza mapema, ambapo Yanga inahusishwa kumuwania nahodha wa Gor Mahia Kenneth Muguna

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu

Muguna anatajwa kuwa kiungo bora katika ligi kuu ya Kenya katika misimu miwili iliyopita

Ni kiungo mshambuliaji mwenye rekodi nzuri ya kufunga mabao ambaye pia hucheza timu ya Taifa ya Kenya

Wakati Mapinduzi Balama akiwa majeruhi, wakongwe Saido Ntibazonkiza na Haruna Niyonzima ndio wachezaji wanaotegemewa zaidi kutengeneza nafasi za mabao pale mbele

Ntibazonkiza amekabiliwa na majeraha mara kwa mara wakati Niyonzima umri unazidi kumtupa mkono, pengine ni wakati kwa Yanga kusaka mbadala wa wachezaji hawa ambaye umri wake bado

Muguna anaweza kuwa chaguo sahihi kuongeza nguvu msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
34m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
59m ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’