Stars yachapwa 4-2 na Zambia

Admin By Admin
β€’
6 Jul 2017
Stars yachapwa 4-2 na Zambia
Licha kutangulia kufunga, timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imeondoshwa kwenye michuano ya Cosafa baada ya kulazwa mabao 4-2 na Zambia katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa Jumatano jioni.

Stars ilitangulia kupata bao la kuongoza kwenye dakika ya 14 mfungaji akiwa Erasto Nyoni aliyepiga mpira wa adhabu nje kidogo ya boksi la 18.

Stars ilicheza vizuri karibu dakika zote za kipindi cha kwanza lakini ni dhahiri uchovu pia kuumia kwa Erasto Nyoni wakati kipindi hicho kikielekea ukingoni kulitoa nafasi kwa Zambia kufunga mabao mawili ya haraka haraka.

Zambia ilitawala mchezo huo kwenye kipindi cha pili na kufanikiwa kupata mabao mengine mawili wakati Stars ilipata bao la pili dakika tano kabla ya mchezo kumalizika, Simon Msuva akiwa mfungaji.

Katika mchezo huo wachezaji wa Stars walionekana kupoteza umakini hasa dakika za mwisho za kipindi cha kwanza na mwanzoni mwa kipindi cha pili.

Pengine uchovu umechangia kwa kiasi kikubwa kwani Stars imecheza michezo mitano ndani ya siku 11 pekee wakati Zambia huo ulikuwa mchezo wao wa pili.

Stars itashuka dimbani keshokutwa Ijumaa kusaka nafasi ya tatu ambapo itacheza na timu itakayofungwa kwenye mchezo wa pili wa nusu fainali kati ya Zimbabwe na Lesotho.

Stars imetumia mashindano haya kujiandaa na mchezo wa kufuzu michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) ikitarajiwa kucheza na Rwanda Julai 15.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’