Baada ya kumaliza majukumu ya timu ya Taifa, kiungo Mukoko Tonombe ameondoka DR Congo kurejea nchini kuendelea na majukumu yake katika klabu ya Yanga
Nahodha huyo msaidizi wa Yanga aliichezea DR Congo kwa mara ya kwanza katika mechi mbili za kuwania kufuzu fainali za Afcon 2021 dhidi ya Gabon na Gambia
Anarejea kukiongezea nguvu kikosi kinachosukwa upya na kocha Juma Mwambusi
Nyota wengine wawili Saido Ntibazonkiza na Haruna Niyonzima pia wako njiani kurejea nchini kuendelea na majukumu yao ngazi ya klabu
ADVERTISE HERE