Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya Afcon 2021, Tanzania sasa inaelekeza nguzu zake kwenye michuano ya kombe la dunia, kampeni ya kusaka tiketi ya michuano ikianza kutimua vumbi mwezi Juni 2021
Tanzania imepangwa kundi J pamoja na timu za DR Congo, Benin na Madagascar
Kulingana na Ratiba ilivyopangwa, michezo miwili itapigwa mwezi Juni dhidi ya DR Congo na Madagascar. Mechi mbili zitapigwa mwezi Septemba dhidi ya Benin na kumaliza hatua ya makundi mwezi Oktoba dhidi ya DR Congo na Madagascar
Ni timu moja tu itakayoongoza kundi ndio itaingia raundi ya mtoano kusaka tiketi ya kushiriki fainali za kombe la dunia zitakazofanyika Qatar mwakani
Afrika ina nafasi tano tu kwenye michuano hiyo mikubwa zaidi duniani
ADVERTISE HERE