Ni wazi hali ilivyo mahusiano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu ya Yanga yameendelea kudorora kutokana na mwenendo wa matukio ya fungia fungia yanayoendelea kuwakumba viongozi wa Yanga
Ni miezi michache iliyopita Kamati ya Maadili ilimfungia Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli kwa kile kilichoelezwa kutoa taarifa za uongo
Leo tena TFF imemfungia Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela miaka mitano kwa tuhuma zinazofanana na zile walizotumia kumfungia Bumbuli
Yanga ina haki ya kulalamika pale inapoona inaonewa. Hizi fungia fungia zina lengo la kutisha na kunyamazisha wale wanaojaribu kuhoji baadhi ya mambo ambayo hayaonekani kufanywa kwa haki
Bila shaka uongozi wa Yanga utakata rufaa kufungiwa kwa Mwakalebela na naamini Kamati ya rufaa itatengua hukumu hizi zinazofanywa kwa 'mihemko'