Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima amesema kuwa licha ya ugumu wa raundi ya pili, hawatakubali kurudia makosa waliyoyafanya kazi michezo ya mwanzo
Niyonzima tayari amerejea kikosini na kuungana na wenzake kujiandaa na mchezo dhidi ya KMC utakaopigwa Jumamosi, April 10 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Niyonzima amesema kwa jinsi walivyojipanga mwaka huu ni wakati wa kumaliza ufalme wa watani zao Simba ambao wametwaa taji la Ligu Kuu mara tatu mfululizo.
"Tuna uzoefu mkubwa na Ligi Kuu Tanzania Bara, mzunguko wa pili umekuwa na hesabu sana na sisi tumejipanga kuhakikisha tunamaliza michezo tukiwa kileleni na kushinda taji," alisema Niyonzima
"Mzunguko wa pili huwa ni mgumu kwani umegawanyika katika sehemu mbili, timu zinazopambana kutwaa ubingwa na zile zinazo pambana kutoshuka daraja hivyo kunaongeza ugumu katika mbio za kulisaka taji lakini tumejipanga kufanya vizuri"
Aidha Niyonzima amesema uwepo wa kocha Juma Mwambusi mwenye uzoefu wa Ligi Kuu ni faida kwao. Wana matumaini makubwa kuwa watashinda ubingwa kama walivyofanya katika msimu wa mwisho wa Mwambusi alipokuwa na kocha George Lwandamina