Migne ni miongoni mwa makocha tunaozungumza nao - Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Apr 2021
Migne ni miongoni mwa makocha tunaozungumza nao - Hersi

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindao Yanga, amesema wanaendelea na mchakato wa kusaka kocha mpya atakayerithi mikoba iliyoachwa na Cedric Kaze

Kumekuwa na tetesi kumuhusu kocha wa zamani wa Harambee Stars na Guinea ya Ikweta Sebastian Migne anayetajwa kumalizana na mabingwa hao wa kihistoria

Hersi amesema Migne ni miongoni mwa makocha wanaofanya nao mazungumzo lakini bado hawajafikia mwafaka

"Ni kweli, Migne ni miongoni mwa makocha ambao tuko katika mazungumzo nao, lakini hayuko peke yake, wengine wapo pia. Bado mwafaka haujafikiwa kuamua yupi tumkabidhi timu, "alisema Hersi

Awali Yanga ilikuwa na mpango wa kumuachia timu kocha Juma Mwambusi mpaka mwishoni mwa msimu

Hata hivyo wamebadili 'gia angani' wakiamua kumleta kocha mpya ambaye atafanya kazi na Mwambusi ili hata pale ligi itakapomalizika atakuwa amefahamu uimara na madhaifu ya timu yako wapi ili imsaidie katika kufanya maboresho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’