Tumeimarika, tuko tayari kwa mapambano - Mwambusi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Apr 2021
Tumeimarika, tuko tayari kwa mapambano - Mwambusi

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Juma Mwambusi amesema ameona mabadiliko kwenye kikosi chake ukilinganisha na wakati alipokabidhiwa timu hiyo mwezi uliopita

Yanga iliachana na kocha Cedric Kaze mwezi uliopita baada ya mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha

Kwa takribani wiki tatu, Mwambusi alijichimbia na vijana wake Kigamboni akiwafua kisawasawa baada ya kubaini hawakuwa 'fiti'

Baada ya mechi mbili za kujipima nguvu, mchezo mmoja ukiwa baina yao Jumamosi iliyopita, Mwambusi amesema vijana sasa wameiva

"Timu imeimarika sana, nimeona kupitia mchezo wa Jumamosi waliokutana wenyewe kwa wenyewe, naona kuna kitu kikubwa kimebadilika sana," Mwambusi alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

"Changamoto ya kutengeneza nafasi na kumaliza ilikuwa ni kubwa sana, tumefanyia kazi hilo. Tuna wachezaji wazuri sana ambao wana kila sababu ya kutwaa ubingwa wa Ligi"

Juzi Yanga ilicheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya African Lyon, vinara hao wa ligi kuu wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0 yaliyofungwa na Fiston Abdul Razak (p), Michael Sarpong na Paulo Godfrey

Aidha, Mwambusi amebainisha kuwa ameongeza wachezaji watatu kutoka timu ya vijana kwa ajili ya kuwajenga na kuwapa nafasi ya kujiamini

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’