Baada ya kukamilika siku 21 za maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, awamu ya tano Hayati Dk John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, shughuli za michezo zinarejea rasmi kuanzia leo ambapo Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea kutimua vumbi kaunzia raundi ya 24
Kulingana na marekebisho ya ratiba yaliyofanywa na Bodi ya ligi, michezo miwili itapigwa leo. Mbeya City watakuwa nyumbani kuikabili Kagera Sugar mchezo ambao utapigwa saa nane mchana
Mchezo utakaofuata saa kumi jioni ni kati ya Namungo Fc dhidi ya Ihefu Fc. Michezo mingine mitatu itapigwa kesho Ijumaa na keshokutwa Jumamosi
Wananchi Yanga watakuwa uwanja Jumamosi kwa mchezo dhidi ya KMC ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa moja usiku

ADVERTISE HERE