Baada ya mapumziko ya takribani mwezi mmoja, kupisha kalenda ya Kimataifa na maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, awamu ya tano hayati Dk John Magufuli, ligi kuu ya Vodacom imerejea leo kwa michezo miwili kupigwa
Mchezo wa mapema ulikuwa kati ya Mbeya City dhidi ya Kagera, mchezo huo ukimalizika kwa suluhu ya bila ya kufungana
Mchezo wa pili ukawashuhudia Namungo Fc wakishindwa kuondoka na alama zote tatu katika uwanja wao wa Majaliwa baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1
Michezo mingine mitatu itapigwa kesho Ijumaa ambapo Biashara United itacheza na Polisi Tanzania, JKT Tanzania itacheza na Mwadui Fc wakati Azam Fc ikicheza na Mtibwa Sugar
Wananchi Yanga ambao wanaongoza ligi hiyo, watashuka dimbani keshokutwa Jumamosi katika mchezo dhidi ya KMC
Mchezo huo utapigwa kuanzia saa moja usiku. Michezo mingine itakayopigwa Jumamosi, Tanzania Prisons itacheza na Dodoma Jiji wakati Gwambina Fc ikicheza na Coastal Union