TFF yainufaisha Simba kuongeza siku dirisha la usajili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Dec 2017
TFF yainufaisha Simba kuongeza siku dirisha la usajili
Simba ndio itakayonufaika zaidi na kuongezwa muda wa dirisha dogo la usajili lililofunguliwa Novemba 15, 2017 na kufungwa Disemba 15, 2017.

Klabu ya Simba inadaiwa bado haijakamilisha usajili wa wachezaji wake wawili wa Kimataifa Asante Kwasi na Dayo Domingues ikielezwa kuwa kuna tatizo la usajili kwenye mtandao wa FIFA, TMS.

Jana TFF ilitangaza kuongeza muda zaidi mpaka Disemba 23 kwa timu kukamilisha usajili.

Baadhi ya mashabiki wa soka wamehoji kilicho nyuma ya maamuzi hayo kwani yametolewa siku moja tu baada ya klabu ya Lipuli kusisitiza kuwa haina taarifa juu ya usajili wa Asante Kwasi kwenda Simba.

Uongozi wa Lipuli umedai Kwasi bado ana mkataba unaozidi miezi sita na timu hiyo hivyo hakupaswa kufanya mazungumzo ya timu yoyote kabla haijawasiliana na uongozi.

"Hapa TFF wanafanya ujanja ujanja tu kuibeba Simba hakuna tatizo la mtandao wala nini," amefunguka shabiki ambaye hakutaka jina lake liwekwe hadharani.

"Haiwezekani uamuzi huo wa kuongeza siku ufanywe baada ya Lipuli kuwasilisha malalamiko kwa TFF kuhusu mchezaji wao Asante Kwasi."

Simba inadaiwa kuwa tayari imevunja mkataba wa aliyekuwa nahodha wake beki Method Mwanjali na mshambuliaji aliyesajiliwa kwa mbwembwe kutoka Ghana Nicolas Gyan.

Inaweza kuathirika kama haitapata beki wa kuchukua nafasi ya Mwanjali iwapo Lipuli itamuwekea pingamizi Kwasi.

Sasa kwa siku zilizoongezwa bila shaka Uongozi wa Simba utaweza kufuata taratibu kwa kumalizana na Lipuli au hata kusajili beki mwingine kama timu hizo hazitafikia makubaliano.

Jambo hilo lisingewezekana kama dirisha la usajili lingefungwa Disemba 15.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’