Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi amesema hali ya kiungo Balama Mapinduzi inaimarika japo awali kulikuwa na sintofamu katika matibabu yake
Balama alirejea mwezi uliopita kutokea Afrika Kusini ambako alifanyiwa matibabu mengine baada ya kubaini uponaji wa jeraha lake ulikuwa na kasoro
"Kulikuwa kuna sintofahamu kwenye matibabu yake kwamba alishatibiwa alifika stage fulani akajitonesha, kwahiyo imebidi aanze upya tena ndio maana unaona alienda kutibiwa Afrika Kusini"
"Sasa hivi hali yake inaendelea kuimarika, kila mmoja wetu, wapenda michezo tumuombee Balama ili apone haraka aweze kurejea katika majukumu yake," alisema Mwambusi
ADVERTISE HERE