Mwambusi afunguka sare ya KMC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Apr 2021
Mwambusi afunguka sare ya KMC

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Juma Mwambusi amesema matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya KMC ni machungu kwao lakini hawana budi kukubaliana nayo kwa kuwa ndivyo mpira wa miguu ulivyo

Huo ukiwa mchezo wake wa kwanza tangu akabidhiwe timu, Mwambusi aliwashuhudia vijana wake wakishindwa kupata ushindi mbele ya watoza ushuru wa Kinondoni katika mchezo ambao walihitaji zaidi ushindi

Akizungumzia tathmini ya mchezo huo, Mwambusi alisema vijana wake hawakucheza vile alivyotaka katika kipindi cha kwanza lakini mabadiliko ya mbinu waliyofanya katika kipindi cha pili yaliwarejesha mchezoni

"Mimi kama Mwalimu nimeyapokea matokeo haya (sare) kwa kuwa ndio ambayo Mwenye ez Mungu ametujaalia, lakini nilihitaji alama zote tatu. Katika kipindi cha kwanza tulicheza chini sana lakini unaona kwenye kipindi cha pili tulibadilika na kusawazisha bao baada ya dakika moja"

"Tulitengeneza nafasi zaidi ya tano nyingine zikiwa za wazi kabisa kama washambuliaji wetu wangekuwa makini pengine tungeondoka na ushindi. Nakiri baadhi ya wachezaji hawakuwa katika kiwango tulichotarajia lakini ndivyo mpira ulivyo tunajipanga kwa mchezo unaofuata," alisema Mwambusi

Bryson David ndiye aliyeitanguliza KMC kwa bao safi kabla ya Yacouba kusawazisha akiunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Saido Ntibazonkiza

Ntibazonkiza atajilaumu kwa kushindwa kutumia nafasi mbili alizopata

Mchezo wa Yanga unaofuata ni dhidi ya Biashara United na itapigwa April 17

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’