Wiki iliyopita klabu ya Simba ilitambulisha basi lao jipya aina ya Tata wakiachana na basi walilopewa mwaka 2012 na waliokuwa wadhamini wao Kilimanjaro Lager ambao pia walikuwa wadhamini wa Yanga wakati huo
Kilimanjaro Lager waliwakabidhi Yanga na Simba mabasi yao Septemba 21, 2012
Ni takribani miaka tisa vilabu hivyo vikongwe vimetumia mabasi hao ambayo kwa hakika sasa yamechoka
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema Yanga ilikuwa na mpango wa kubadili basi lake na sasa wanakaribia kushusha basi hilo jipya
Bumbuli amewataka wapenzi wa wanachama wa klabu ya Yanga watulie kwani wanaleta basi kali kuliko waliloleta watani zao Simba
"Yanga tupo katika mpango wa kushusha basi jipya kali kuliko lile Tata la wenzetu (Simba), sio kwamba mpango huu ni baada ya kuona wenzetu wameanza, hapana, bali ni mpango ambao tumekuwa nao kwa muda mrefu"
"Hivyo wapenzi wa Yanga wanatakiwa kutulia kwani tutashusha basi jipya na kali kwa ajili ya safari za wachezaji za hapa na pale," amesema Bumbuli
Yanga na Simba ni kama 'mapacha' hivyo ni suala la muda tu Yanga nao watatambulisha basi jipya