Beki wa kushoto wa Yanga Yassin Mustafa anaendelea kukosekana kikosini akiwa bado ni mgonjwa
Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Juma Mwambusi amesema Yassin na kiungo Mapinduzi Balama hawatakuwa sehemu ya kikosi chake kitakachoivaa Biashara United siku ya kesho Jumamosi katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa moja kamili usiku
"Wachezaji wako tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Biashara United ingawa wapo wachezaji ambao tutawakosa kesho. Yassin ni mgonjwa wakati Balama (Mapinduzi) ni majeruhi," alisema Mwambusi
ADVERTISE HERE