Match Day : Yanga vs Biashara United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Apr 2021
Match Day : Yanga vs Biashara United

Mikiki mikiki ya ligi kuu ya Vodacom inaendelea leo katika viwanja tofauti ambapo jijini Dar es salaam vinara wa ligi hiyo Yanga watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikaribisha Biashara United

Ni mchezo ambao Yanga inahitaji alama zote tatu ili kuweka hai matumaini ya kuwania ubingwa msimu huu

Wachezaji wa Yanga wanafahamu matokeo tofauti na ushindi, yanaweza kuwapa nafasi watani zao Simba kuwaondoa kileleni kesho watakapocheza na 'vibonde' Mwadui Fc mkoani Shinyanga

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Juma Mwambusi amesema mchezo wa leo ni mwanzo mpya kwao baada ya mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha

Amesema wanahitaji kushinda leo ili kurejesha morali ya ushindi katika kikosi lakini pia kuhakikisha wanashinda michezo yote 10 iliyobaki kumaliza msimu

Mwambusi atakuwa na kikosi chake kamili akiwakosa wachezaji wawili tu, Yassin Mustafa na Mapinduzi Balama

Kiungo mshambuliaji Carlos Carlinhos leo anaweza kurejea kikosini baada ya kumaliza adhabu ya kadi nyekundu iliyomfanya akose michezo mitatu iliyopita

Mashabiki wa Yanga wameaswa kusahau yaliyopita, wajitokeze kwa wingi kuiunga mkono timu yao katika mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa moja usiku

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
12m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’