Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amewaalika mashabiki kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia burudani itakayo ambatana na ushindi kutoka kwa timu yao
Huu ni mchezo ambao hakuna matokeo mengine zaidi ya ushindi ambayo Wananchi wanayahitaji
Benchi la ufundi, viongozi na wachezaji wanafahamu umuhimu wa ushindi katika mchezo huu utakaopigwa kuanzia saa moja kamili usiku
Sapoti ya mashabiki itaongeza hamasa kwa wachezaji ambao wameahidi kuwa leo hawatawaangusha
Nugaz anasema Yanga inakwenda kumaliza mchezo huo mapema tu
"Wanachama, wapenzi na Mashabiki tujitokeze kwa wingi leo saa moja kamili usiku uwanja wa Mkapa tumalize ngebe za Biashara United mapemaaaa"
ADVERTISE HERE