Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Juma Mwambusi amesema ameridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na timu yake katika mchezo dhidi ya Biashara United
Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Benjamini Mkapa, uliishuhudia Yanga ikiondoka na ushindi wa bao 1-0 na kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufiksha alama 54
Akizungumza baada ya mchezo huo, Mwambusi alisema ulikuwa ni mpango wao kucheza soka la kushambulia ilikutengeneza nafasi na kuzitumia ili kuondoka na ushindi

"Kama nilivyoahidi kuwa tutacheza soka la kushambulia tangu mwanzo, tumetengeneza nafasi nyingi na tumeweza kuitumia moja. Muhimu zaidi tumefanikiwa kuondoka na alama zote tatu"
"Nilieleza mchezo uliopita wachezaji hawakuwa katika ubora wao sababu tulitoka kwenye mapumziko. Lakini leo niliwaambia kuwa tunapaswa kucheza kama klabu ya Yanga"
"Sikuwa na shaka na wachezaji nilioanza nao, nawaamini wachezaji wangu wote na niliwaeleza kila mmoja atapata nafasi kulingana na juhudi zake. Kwa kiasi kikubwa wachezaji wamefuata kile tulichowaelekeza," alisema Mwambusi
Yanga itaendelea kubaki jijini Dar es salaam ambapo keshokutwa Jumanne watashuka tena uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Gambina Fc