Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima amesema wako tayari kuikabili Gwambina Fc katika mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa kesho Jumanne katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Niyonzima amesema Yanga imedhamiria kushinda kila mchezo ili kuhakikisha hawapotei katika mbio za kuwania ubingwa msimu huu
"Tumejianda vizuri na tunaamini mchezo wa kesho utakuwa mgumu ila sisi kila mechi tunahitaji alama tatu (3) kama tulivyosema hapo awali na tunaamini mchezo wa kesho utakuwa mzuri kwa upande wetu"
"Tangu nimeanza kucheza soka hapa Tanzania, Yanga haijawahi kukaa misimu mitatu bila ya kushinda ubingwa, hivyo utaona iko presha kubwa kwa wachezaji kuhakikisha tunafanya vizuri. Lakini hili ni jambo la kawaida ambalo sisi wachezaji tunajua vile tunaweza kukabiliana nalo," alisema Niyonzima
Nae Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Juma Mwambusi amesema wataingia katika mchezo huo kwa tahadhari kubwa kwani wanafahamu Gwambina Fc sio timu ya kubeza
"Tunajua ni mchezo mgumu na hatuwezi kuwabeza Gwambina Fc kutokana na nafasi waliyopo na ukizingatia ushindani wa ligi ni mkubwa msimu huu na wao ni moja kati ya timu bora"