Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United, leo Yanga imepania kuendeleza wimbi la ushindi itakapoikabili Gwambina Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Mchezo huo utapigwa kuanzia saa moja kamili usiku
Huo utakuwa mchezo wa tatu kwa Kaimu Kocha Mkuu Juma Mwambusi ambaye amefanikiwa kukusanya alama nne kutoka michezo miwili
Mwambusi amesema wamejipanga kuondoka na alama zote tatu licha ya kuwa wanafahamu mchezo hautakuwa mwepesi
Baadhi ya wachezaji watakosekana kutokana na sababu mbalimbali
Feisal Salum, Yassin Mustafa na Mapinduzi Balama ni majeruhi wakati nahodha Lamine Moro atapewa mapumziko ili kupona majeraha madogo aliyokuwa amepata mazoezini
Mwambusi huenda akakirudisha uwanjani kikosi kilichopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United katika mchezo uliopita
Yanga inahitaji kushinda mchezo huo ili kuendelea kubaki katika mbio za kuwania ubingwa wa msimu huu