Yanga leo imecheza mechi nzuri sana ikifanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Gwambina Fc
Mabadiliko yameanza kuonekana katika kikosi, timu inacheza kwa mipango, pongezi nyingi kwa kiungo Carlos Carlinhos
Carlinhos ameongeza ubunifu katika eneo la kiungo
Kaimu Kocha Mkuu Juma Mwambusi amefanikiwa kuondoka na alama saba kati ya tisa pale katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Jumapili anakabiliwa na mchezo mwingine dhidi ya Azam Fc
Huu ni mchezo muhimu sana, alama tatu zitaiweka Yanga katika nafasi nzuri katika mbio za kuwania ubingwa
Lakini pia ushindi utaiongezea timu morali kuelekea mchezo wa kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa wiki ijayo mkoani Rukwa
ADVERTISE HERE