Uongozi wa klabu ya Yanga umethibitisha kuwa wamelipa deni la aliyekuwa mshambuliaji wao Amissi Tambwe ambaye aliwashitaki FIFA
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wamelipa kiasi cha Tsh Milioni 52 ambapo mchanganuo wake ni; Tsh Milioni 48 alilipwa Tambwe na Tsh Milioni 3.7 zililipa gharama za Mawakili
Hivyo ni rasmi Yanga imeepuka kifungo walichokuwa wamewekewa na FIFA kama wasingelipa deni hilo
Wakati Wananchi wakilipa madeni, watani zao Simba wao wamekumbana na rungu la FIFA baada ya kushindwa kumlipa Asante Kwasi raia wa Ghana
Simba wamefungiwa kusajili kwa mwaka mmoja baada ya kushindwa kulipa kiasi cha Tsh Milioni 9
ADVERTISE HERE