Huyu mwamba apewe muda, atafanya kitu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Apr 2021
Huyu mwamba apewe muda, atafanya kitu

Kocha Mpya wa Yanga Nasredinne Nabi jana alianza rasmi majukumu ya kukinoa kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria ikiwa ni siku mbili tangu alipotua nchini

Nabi ameanza majukumu yake huku akipata usaidizi kutoka kwa kocha Juma Mwambusi ambaye imeelezwa ataendelea kubaki kikosini mpaka mwishoni mwa msimu

Nabi ataanza kuonekana uwanjani baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc pale vibali vyake vya kufanya kazi nchini vitakapokuwa vimepatikana

Msimu huu Yanga ilianza na Zlatko Krmpotic, akafuata Cedric Kaze, Juma Mwambusi na sasa Nabi, ni makocha wanne mpaka sasa

Yanga ilikuwa katika presha kubwa ya kusaka ubingwa, haishangazi kuona mabadiliko hayo yalifanyika kila wakati timu iliposuasua

Nabi ameletwa kwa mpango wa muda mrefu, bila shaka kocha huyo raia wa Tunisia atapewa muda aweze kuifanya kazi yake

Malengo yaliyowekwa msimu huu ni kushinda ubingwa wa VPL, bado Yanga ina nafasi ya kufanya hivyo lakini isiwe kigezo cha kibarua cha Nabi kwani yeye ataiongoza timu katika michezo nane tu

Katika Mkutano aliofanya na Wanahabari baada ya kusaini mkataba, Nabi alisema timu inahitaji kuimarishwa baadhi ya maeneo kiufundi hivyo ataifanya kazi hiyo

Mashabiki wa Yanga hawapaswi kumuweka katika presha kubwa Nabi ambaye kabla ya kutua Yanga aliinoa klabu ya El Merrikh kwa muda mfupi

Nabi alisisitiza kuwa anahitaji kupewa muda aifanye kazi yake kwa ufasaha

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
53m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’