Yale mambo yaliyojitokeza mchezo uliopita dhidi ya Gwambina Fc yalimalizika palepale uwanjani, mwamba Saido Ntibazonkiza yuko tayari kuwavaa Azam Fc katika mchezo utakaopigwa saa mbili na robo usiku leo Jumapili
Ntibazonkiza ni silaha muhimu ya Yanga katika mchezo huo. Ndiye mchezaji mwenye madhara zaidi kila anapokuwa dimbani
Katika michezo yote aliyoitumikia Yanga tangu aliposajiliwa mwezi Januari, ni mchezo mmoja tu dhidi ya Biashara United ndio hakuhusika kutengeneza au kufunga bao
Ana assist nne na mabao matatu mpaka sasa. Uzoefu wake utakuwa chachu kwa Yanga kufanya vizuri katika mchezo dhidi ya Azam unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali
Azam Fc walifungwa katika mchezo wa kwanza uliopigwa Azam Complex hivyo leo wanatarajiwa kuja kivingine
Lakini pia katika mchezo wa kwanza, Ntibazonkiza hakuwepo, bila shaka leo atakuwepo