Mwenendo huu ni mateso kwa mashabiki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Apr 2021
Mwenendo huu ni mateso kwa mashabiki

Matokeo yasiyorishisha ambayo Yanga wanapata, yanawaumiza sana mashabiki

Hamasa ilikuwa kubwa kuanzia mwanzo wa msimu, mashabiki wakajenga imani kuwa msimu huu kuna kitu kitafanyika

Lakini Yanga imepoteza makali yake mwishoni kabisa mwa mbio wengi wanajiuliza nini kimeikumba timu yao pendwa?

Kwa hakika huu ni msimu mwingine ambao Wanayanga wanakosa raha kutoka kwa timu yao

Wengi wanajiuliza, ule ubora ambao Yanga ilianza nao msimu umepotelea wapi?

Pamoja na mabadiliko ya benchi la ufundi, ni kama timu imeendelea kupoteza makali siku hadi siku

Wapo wanaoamini kuwa mabadiliko yaliyofanyika karibuni ni kama yameivuruga timu tu, kulikuwa na ulazima gani wa kuleta kocha mpya wakati msimu uko mwishoni?

Mbona Juma Mwambusi alikuwa ameanza kuiimarisha timu, ile ahadi ya kumuacha mpaka mwisho wa msimu iliishia wapi?

Kwa hakika viongozi wa Yanga wana cha kuwaambia Wanachama katika Mkutano Mkuu ambao utafanyika mwezi ujao

Wao ndio walipewa dhamana ya kuisimamia timu lakini mpaka sasa wanachoambulia ni maumivu tu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
37m ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
10h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
15h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
19h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
20h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
20h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’