Mchezo wa mzunguuko wa pili kombe la FA kati ya Yanga dhidi ya timu ya daraja la pili, Reha FC utapigwa Disemba 24 kwenye dimba la Uhuru.
Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa kumi kamili jioni.
Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo na watahakikisha wanapata ushindi ili kusonga mbele.
Amesema Yanga haitadharau wapinzani wao kwa kuwa anaamini timu yoyote iliyopata nafasi kutinga kwenye michuano hiyo ina uwezo.
Kikosi cha Yanga kimeendelea kujifua kwenye dimba la Uhuru kujiandaa na mchezo huo.

ADVERTISE HERE