Pato atamani kurejea Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Apr 2021
Pato atamani kurejea Yanga

Nahodha Msaidizi wa klabu ya Polisi Tanzania Pato Ngonyani amesema shinikizo la matokeo na matarajio makubwa kutoka kwa mashabiki vilimfanya ashindwe utamba wakati akiitumikia Yanga

Pato aliondoka Yanga msimu uliopita akajiunga na Polisi Tanzania ambapo amekuwa na msimu mzuri katika kikosi cha maafande hao

Pato amebainisha kuwa sasa anacheza vizuri sababu ya kuaminiwa na hana shinikizo kama ambavyo ilikuwa awali wakati anaitumikia Yanga

Kiraka huyo anayeweza kucheza nafasi ya kiungo mkabaji na mlinzi wa kati, amesema sasa amekomaa na yuko tayari kurejea kwa Wananchi au timu yoyote itakayomuhitaji na kukubaliana nayo pale mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu

"Uzoefu niliopata wakati nikiwa Yanga umenifanya kuwa mkomavu na nimeaminiwa na benchi la ufundi la Polisi Tanzania na kuniona nafaa kuwa nahodha msaidizi,'" alisema Pato

"Mpira ni maisha yangu, kama Yanga au timu nyingine yoyote itanihitaji, niko tayari kujiunga nayo muhimu tu kuwe na maslahi"

Pato aliitumikia Yanga kwa takribani misimu minne kabla ya kutolewa kwa mkopo klabu ya African Lyon dirisha dogo msimu wa 2018/19 na baadae Polisi Tanzania ikamsajili akiwa mchezai huru

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
2h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
10h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
11h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
14h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’