Wananchi wametinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho kibabe kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons
Bao la Yacouba Songne akimalizia pasi mpenyezo ya Saido Ntibazonkiza ilitosha kuwahakikishia Yanga ushindi muhimu
Prisons waliingia katika mchezo huo wakiwa wamekamia lakini utulivu wa wachezaji wa Yanga uliwafanya watawale mchezo kwa muda mwingi huku Prisons wakicheza 'pira gwaride'
Wajelajela wamepigwa hapo hapo katika uwanja wao na imekuwa ngumu kwao kukubali matokeo
Wananchi wanarejea Dar kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa May 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa



ADVERTISE HERE