Katika michezo ambayo Yanga imecheza kwa nidhamu kubwa, mchezo dhidi ya Tanzania Prisons leo ni miongoni
Pamoja na kukutana na mazingira magumu dhidi ya Prisons ambao wanafahamika kwa aina ya soka wanalocheza, Yanga ilikuwa bora sana
Mipango ya mashambulizi ilionekana, kama kungekuwa na umakini, mabao zaidi yangefungwa
Abdallah Shaibu 'Ninja' ameendelea kuinogesha safu ya ulinzi wakati Carlinhos nae amedhihirisha anaweza kucheza soka la aina yoyote
Pamoja na kuvamiwa mara kwa mara na wachezaji wa Prisons, Carlinhos alikuwa mchezaji hatari zaidi katika kipindi cha kwanza kabla hajaumizwa na kulazimika atolewe mapema katika kipindi cha pili
Ipo kazi ambayo kocha Nesreddine Nabi ameifanya, Yanga iliyocheza leo ni tofauti kabisa na ile iliyocheza mchezo uliopita dhidi ya Azam Fc
Wananchi wana kila sababu ya kuwa na imani, May 08 kuna watu maji wataita 'Mma'
Muhimu kwa mashabiki ni kuendelea kuiunga mkono timu yao huku wakifahamu ujio wa Nabi ni kwa ajili ya kutengeneza timu ya ushindani zaidi
Kazi hiyo ameianza na taratibu kuna mambo yameanza kuwaingia wachezaji