Uongozi wa klabu ya Yanga umemtaka nahodha wa Tanzania Prisons Benjamin Asukile athibitishe tuhuma alizotoa dhidi ya Yanga baada ya mchezo wa hatua ya 16 bora kombe la FA ambao Yanga ilishinda bao 1-0 hapo jana
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema hawatakubali kuchafuliwa na watamshitaki mchezaji huyo kwa Mamlaka husika
"Nahodha wa Tanzania Prisons Benjamin Asukile ametoa tuhuma mzito dhidi ya Yanga
1. Amesema tuliwazidi kwa sababu tulimuongeza Refa upande wetu, Hili tunataka alithibitishe, Kivipi na kwa namna gani!?
2. Walikuwa wakiwapigia simu na kutaka kutoa Mil 40 (Rushwa) I'll watuachie game, hili pia tunataka alithibishe mbele ya ya Mamlaka husika.
Hakuna namna ambayo Yanga tunaweza kuvumilia kuchafuliwa kwa kiwango hiki. Asukile anasahahu kwamba ushindi pekee ambao Timu yake imewahi kuupata tangu msimu wa 2018/19 hadi sasa ni sare tatu tu katika mechi Nane.
Msimu wa 2018/19 tuliwafunga mabao 3-1 kwao, pia tukawafunga 2-1 kwa Mkapa. Msimu wa 2019/20 tuliwafunga 1-0 kwao (Samora), wakaambulia sare kwa Mkapa na tukawatoa kwenye FA kwa mabao 2-0.
Msimu huu wamebahatika kupata sare mechi zote mbili za Ligi, na Jana wamekaa kwao, sasa huo ujasili wa Asukile na kujitoa ufahamu kuona wao ni wababe ameutoa wapi?
Tutazifikisha tuhuma hizi zote kwa Mamlaka husika ASAP"