Kumbe ni ndugu moja...!

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 May 2021
Kumbe ni ndugu moja...!

'Basi tukutane kwa Mkapa Jumamosi ijayo halafu tutatukana tena hapohapo baada ya wiki mbili'

Ni kauli za mashabiki wa Yanga baada ya watani zao Simba kupangwa kucheza na Kaizer Chiefs katika mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa

Pale Afrika Kusini Kaizer Chiefs ni timu ya 'wazawa' kwa huku kwetu unaweza kuifananisha na Yanga kuwa timu ya Wananchi

Kule dabi yao ni dhidi ya Orlando Pirates 'mabwanyenye' ambao huku kwetu unaweza kuwafananisha na Simba

Chiefs ndio timu yenye mataji mengi zaidi Afrika Kusini wakishinda mataji 93 katika miaka 47

Wanatumia uwanja wa FNB ambao unachukua takribani mashabiki 94,000 kama isingekuwa corona, uwanja huo 'ungetapika' katika mchezo wao dhidi ya Simba

Mwaka jana Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga, Mhandisi Hersi Said alitembelea klabu hiyo katika mpango wa kujenga ushirikiano

Ni hivi karibuni tu Chiefs nao wakafika kuitembelea Yanga kujifunza mambo mbalimbali pamoja na kuimarisha ushirikiano hasa katika kukuza soka la vijana

Timu hizi zina rekodi zinazoshabihiana, kama ilivyo historia ya Afrika Kusini na Tanzania, basi ndivyo ilivyo Kaizer Chiefs na Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’