Baada ya kurejea kutoka Sumbawanga mwishoni mwa wiki, kikosi cha Yanga kilielekea moja kwa moja kambini Kigamboni kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba
Mchezo huo wa ligi kuu utapigwa Jumamosi, May 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mkongwe na mmoja wa manahodha wa kikosi cha Yanga Haruna Niyonzima amesema wanajipanga kuhakikisha wanashinda mchezo huo
Niyonzima amebainisha kuwa Yanga haijakata tamaa na mbio za ubingwa, wanafahamu wanahitaji kupata matokeo katika kila mchezo unaokuja mbele yao
"Mchezo wetu dhidi ya Simba mara nyingi huwa mgumu sana, lakini soka lina matokeo matatu ambayo ni kushinda, kushindwa na kutoka sare, mwalimu ametueleza nini anataka wachezaji wote tunajua kwamba utakuwa mchezo mgumu, tumejipanga kufanya vizuri, " alisema
Niyonzima alisema mbinu walizopewa na Kocha wao Mkuu, Nassredine Nabi ambaye amekuwa akiwasisitiza kuongeza umakini kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu katika kila mchezo ili kuongeza presha kwa Simba waliopo kileleni