Hakuna kitu kizuri kama Mwalimu kutambua kazi unayofanya uwanjani na kukuhamasisha uiendeleze zaidi
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ameonyesha imani kubwa kwa mlinzi Abdallah Shaibu 'Ninja'
Hii ni silaha yake muhimu kuelekea mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi
Ninja alirejeshwa kwenye kikosi cha kwanza na aliyekuwa kocha wa muda Juma Mwambusi
Kocha huyo raia wa Tunisia, ameendelea kumtumia katika michezo miwili iliyopita
Ni mchezaji aliye katika kiwango bora sana, ingekuwa maajabu kama asingemtumia
Mchezo dhidi ya Simba Jumamosi ni muhimu kwa Yanga kushinda ili kuendelea kuweka hai matumaini ya kuwania ubingwa msimu huu
Safu bora ya ulinzi siku zote itakuhakikishia kushinda mataji, Yanga imeonyesha mabadilko makubwa katika eneo la ulinzi katika michezo ya karibuni
Hakuna wasiwasi kabisa na eneo hilo kuelekea mchezo dhidi ya Simba.
Kibwana, Adeyum, Ninja, Lamine Moro, Bakari Nondo Mwamnyeto, Dickson Job na Said Juma Makapu wote wapo tayari