Jumamosi ya wiki hii nyasi za uwanja wa Benjamin Mkapa zitawaka moto wakati mabingwa wa kihistoria Yanga watakuwa uwanjani kuwakabili watani zao, Simba ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom
Katika mchezo huo Yanga watakuwa wageni, muda wa mchezo ukipangwa kupigwa saa 11 jioni
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema wanahitaji kuwapa furaha mashabiki kwa kupata matokeo chanya pia akiwataka kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
"Furaha yetu ni kuona timu inapata matokeo chanya na kucheza Mpira vizuri, hivyo basi ni jukumu letu wanachama, wapenzi na Mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa hamasa timu yetu ili kuhakikisha inapata matokeo siku ya Jumamosi ya tarehe 08/05/2021 dhidi Simba Sc"
ADVERTISE HERE