Jumamosi hii, May 08 2021 nyasi za uwanja wa Benjamin Mkapa zitawaka moto pale miamba wa soka nchini Simba na Yanga watakapoumana katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Viingilio vya mchezo huo vimewekwa hadharani ambapo Mzunguuko ni Tsh 7,000/-, Orange Tsh 10,000/-, VIP B ni Tsh 20,000/- na VIP A ni Tsh 30,000/-
Simba ndio wenyeji wa mchezo huo ambao utapigwa kuanzia saa 11 jioni
Vituo ambavyo unaweza kujipatia tiketi hizo ni pamoja na Dar Live (Mbagala), Maduka ya Vunjabei yaliyopo Sinza na Kinondoni, uwanja wa Mkapa, Big Bon (Sinza), Sheli ya Engen Mwembeyanga, Ofisi za TFF Karume, Sandaland (Kariakoo), Shaffih Dauda Sports Wear (Sinza na Tabata) na Buguruni Sheli
Mchezo huo pia utakuwa mbashara kupitia Azam Sport 1 HD
ADVERTISE HERE