Mukoko Tonombe ni mmoja wa wachezaji ambao Yanga inajivunia kuwa nae kuelekea mchezo wa dabi dhidi ya Simba ambao utapigwa keshokutwa Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Katika mchezo wa duru ya kwanza uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1, Mukoko ndiye aliyeondoka na tuzo ya nyota wa mchezo
Kiungo huyo wa zamani AS Vita, ana uzoefu wa kucheza mechi kubwa, mchezo dhidi ya Simba hauwezi kumsumbua
Ni mwezi uliopita tu ametokea kuitumikia timu ya Taifa ya DR Congo, ambayo sio rahisi kupata nafasi ya kucheza kutokana na wingi wa nyota wanaosakata kabumbu barani Ulaya
Mukoko alifanikiwa kucheza mechi zote mbili
Kwa asili ni kiongozi, muda wote anapokuwa uwanjani anazungumza na wenzake kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri
Wananchi hawawezi kuwa na hofu kuelekea mchezo wa Jumamosi hasa wakiwa na wachezaji aina ya Mukoko