Yanga imepongezwa kwa maamuzi ya kutoa timu uwanjani jana baada ya TFF kukiuka kanuni walizozitunga wao wenyewe na kujaribu kulazimisha mabadiliko ya muda wa mchezo masaa mawili kabla ya mchezo kupigwa
Yanga ilipeleka timu saa 11 jioni na kusubiri kwa takribani dakika 15 kama kanuni zinavyoelekeza na baadae kuondoka uwanjani hapo
Wabunge, wanasiasa, viongozi wa dini na wananchi wa kawaida wametoa matamko mbalimbali ya kupongeza msimamo ulioonyeshwa na Yanga 





Maandalizi ya mchezo huo yalianza takribani wiki tatu zilizopita
Hata katika kikao cha mchezo kilichofanyika asubuhi hakukuwa na Mabadiliko yoyote ya muda wa mchezo yaliyofanywa
TFF wenyewe kupitia kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii waliweka tangazo la kusisitiza kuwa mchezo huo utapigwa saa 11 jioni
Kwa wale waliitumia hoja ya uzinduzi wa kitabu cha Rais Mstaafu Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi, tukio hilo pia lilifahamika lingefanyika jana
Hivyo kama hiyo ndio sababu TFF walikuwa na muda wa kuzingatia kanuni zao kwa kuziarifu timu kuhusu mabadiliko hayo saa 24 kabla ya mchezo