Anaandika Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli;
Fahamu Madaraja Mawili ambayo ni gumzo hapa nchini
1. Daraja la Mwl. Nyerere a.k.a Daraja la Kigamboni Daraja hili lina upana wa mita 27.5 sawa na futi 90 ambao imeliwezesha kuwa na njia sita za kupita magari, (6 lanes dual carriageway), lina urefu wa mita 680 sawa na futi 2,230. Daraja la Kigamboni linakatisha Bahari ya Hindi.

2. Daraja la Mkapa Hili ndio Daraja refu zaidi kwa sasa hapa Tanzania, likiwa na mita 970 sawa na futi 3,180, na upana wa mita 10.3 likiwa na njia mbili (2 lanes). Daraja hili linakatisha katika mto Rufiji.

Madaraja mengine mawili ambayo Serikali inaendelea na ujenzi wake ni Daraja jipya la Silander (Salenda), na Daraja la Kigongi Busisi
ADVERTISE HERE