Timu imeimarika, tungewashangaza - Senzo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 May 2021
Timu imeimarika, tungewashangaza - Senzo

Mshauri wa Yanga Senzo Mazingisa amesema mabingwa hao wa kihistoria walijipanga kuwakabili watani zao Simba, walikuwa tayari kuwapa furaha mashabiki wao

Senzo amesema hawakufurahishwa na kile kilichotokea kupelekea mchezo huo kushindwa kufanyika, wanasubiri maamuzi yatakayofikiwa na wenye mamlaka ya usimamizi wa soka nchini

Aidha Senzo amesema yapo mabadiliko ya kiuchezaji kikosi cha Yanga kinaonyesha sasa tangu ujio wa kocha mpya Nasreddine Nabi

"Timu yetu imeanza kuimarika sana, ni bahati mbaya mchezo wa Simba uliahirishwa, lakini wanachama na mashabiki wangeona kitu tofauti,  wachezaji wameanza kumuelewa kocha kwa kiasi kikubwa," alisema Senzo

Senzo ameongeza kuwa kwa sasa mawazo yao yote ni kuelekea mchezo dhidi ya Nambungo Fc ambao utapigwa Jumamosi, May 15 katika uwanja wa Majaliwa, Lindi

"Mchezo hautakuwa mwepesi, lakini kwa sasa tuna kikosi ambacho ukiongeza mbinu za Mwalimu, mashabiki watarajie kuona kitu tofauti hasa kuongezeka kwa ubora wa mbinu"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
23h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’